Upasuaji mara 13 afanane na Ivanka Trump…kisa??
Lakini duniani isivyoishiwa na mambo wapo ambao hufikiria kufanana na watu maarufu hata hufikia hatua ya kufanya upasuaji kwa ajili ya kufanana na watu wanaowapenda.
Sasa stori iliyonifikia ni kwamba Mwanamke mmoja wa Marekani anayeitwa Tiffany ameweka hadharani nia yake ya kujibadili mwili wake kwa upasuaji ili afanane na mtoto wa kwanza wa Rais wa Marekani Donald Trump, Ivanka Trump.
Tiffany ameweka wazi kuwa hadi wakati huu ameshafanyiwa upasuaji mara 13 ndani ya mwaka mmoja ili afanane na Ivanka na anaamini alikua mrembo zamani lakini pia mwonekano wake mpya ni mzuri zaidi.
Kabla ya upasuaji Tiffany alikuwa na nywele ndefu za kahawia lakini upasuaji huo umefanya nywele zake ziwe ‘blond’ na tangu aanze safari yake hiyo amekwishafanya mabadiliko kwenye sehemu za kifua, pua, macho, mdomo, tumbo pamoja na makalio.
Nini kilichomfanya Tiffany kutaka kufanana na Mjasiriamali huyo? Ni kwa sababu anaamini Ivanka ni “role model kwa wanawake wote.”
No comments:
Post a Comment