Bomu kubwa la vita vya pili vya dunia kuharibiwa Ujerumani
Karibu watu 65,000
wakazi wa mji Frankfurt wamendoka makwao kutoa nafasi kwa wataalamu
wanaoharibu bomu kubwa ambalo lilikosa kulipuka wakati wa vita vya pilia
vya dunia.
Polisi wanasema kuwa shughuli ya kuharibu bomu hilo
ilianza kufuatia kuhamishwa watu wengi zaidi katika historia ya
Ujerumani baada ya vita.Maeneo yaliyohamishwa watu ni pamoja na hospitali, makao ya watu wazee na benki kuu ya Ujerumani
Inaaminika kwa kuna maelfu ya mabomu ambayo hayakulipuka nchini Ujerumani.
Wenyeji wengi walisema kuwa wangetumia muda wao mwingi siku ya leo kutembelea familia, kuzuru sehemu tofauti za mjii hadi itakapobainika kuwa eneo hilo liko salama.
No comments:
Post a Comment