Rapper Chid Benz akamatwa na Polisi akiwa na Dawa za Kulevya
Moja ya taarifa kubwa inayosambaa kwenye mitandao tangu jana ni hii inayomuhusu Rapa Chid Benz na wenzake Sita kukamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala wakiwa na dawa za kulevya baada ya kufanya msako.
Hivi karibuni ilielezwa kuwa Chid Benz alikuwa ameanza kurejea katika kazi zake za kisanii baada ya kutoa wimbo wake ‘Muda’ aliomshirikisha Q Chief akielezea mateso aliyopitia wengi wakiamini kuwa ameacha kutumia dawa hizo na kuanza kushiriki matamasha mbalimbali ya muziki huku afya yake ikionekana kuimarika.
Kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM leo August 16, 2017 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amethibitisha na kusema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12, 2017 majira ya saa 11:50 Jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya>>>”Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha Msimbazi, tunaendelea na upelelezi, ukikamilika tutawafikisha Mahakamani. Dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu na itajulikana ni kiasi gani cha dawa za kulevya zilizokamatwa.” – Hamduni.

No comments:
Post a Comment