PICHA 9: Polisi wakabiliana na waandamanaji Kenya; Moto Kuwashwa Barabarani
Polisi kupambana na fujo wakijaribu kuzima maandamano katika ngome ya upinzani katika mtaa wa Mathare, Nairobi.
Polisi wamekuwa wakisaidia pia kuzima maandamano mjini Kisumu ambapo baadhi ya wakazi walikuwa wamefunga barabara na kuwasha moto matairi.
Waziri apuuzia mbali madai ya maandamano na fujo
Amesema taarifa hizo hazina msingi wowote.
"Iwapo kungekuwa na jambo, mkuu wa polisi ndiye huyu hapa angekuwa wa kwanza kujua," amesema Dkt Matiang'i.
Kisumu, magharibi mwa Kenya muda mfupi uliopita polisi wamekabiliana na vijana waliokuwa wakiandamana katika barabara ya Manyatta katika mtaa wa Kondele na eneo la Kibos.
Odinga: Mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa
Mgombea
urais wa muungano wa upinzani Nasa Raila Odinga amewaambia wanahabari
kwamba wamepata habari kwamba mitambo ya Tume ya Uchaguzi IEBC
ilidukuliwa na matokeo halisi kufanyiwa ukarabati.
Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC.
Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake.
Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.
Bw Odinga, amesema huo ulikuwa "ulaghai wa hali ya juu".
Hata hivyo, ametoa wito kwa wafuasi wa muungano huo waendelee kuwa watulivu.
Bw Musyoka amesema anawashauri wafuasi wa muungano huo waendelee na shughuli zao za kawaida, ingawa huenda karibuni wakatakiwa kuchukua hatua.
Bw Odinga na Kalonzo wamekataa kusema ni hatua gani zaidi watachukua na badala yake wakasema wanasubiri kusikia ufafanuzi kutoka kwa IEBC kuhusu yaliyotokea.

Chebukati: Tutachunguza madai ya Nasa kuhusu udukuzi
Mwenyekiti
wa IEBC Wafula Chebukati amewaambia wanahabari baadaye kwamba wamepata
habari kuhusu tuhuma za muungano huo wa upinzani kwamba mitambo yao ya
uchaguzi ilidukuliwa.
Amesema tume haiwezi kupuuza tuhuma kama hizo na kwamba maafisa wake watafanya uchunguzi kubaini iwapo kuna ukweli wowote katika madai hayo.
Hata hivyo alieleza imani yake kwamba mfumo wa uchaguzi unaotumiwa na tume hiyo ni imara na kwamba ulitumiwa na shughuli zote za awali, na sasa "imesalia shughuli ya mwisho" ya kupeperusha na kutangaza matokeo ya kura.

No comments:
Post a Comment