Souare arejea dimbani baada ya Mwaka
Beki wa Crystal
Palace Pape Souare amerejea uwanjan toka alipopata ajali mbaya ya gari
na kusababisha kuvunjika mfupa wa nyonga na taya.
Souare mwenye
umri wa miaka 27 alipata ajali ya gari mwezi Septemba mwaka 2016 na
alirejea mazoezi na klabu yake mwanzoni mwa mwezi huu.Mlinzi huyo wa kulia raia wa Senegal alicheza kwa dakika arobaini na tano akiwa na kikosi cha chini ya umri wa miaka 23 cha timu yake dhidi ya Nottingham Forest.
Crystal Palace walipoteza mchezo huo kwa kufungwa kwa mabao 2-1 na baada ya mchezo Souare aliandika katika ukurasa wake wa mtandao Twita " Nina furaha kupata dakika kadhaa kucheza nahisi vizuri."


No comments:
Post a Comment