Baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii na picha zikisambaa kutoka uwanja wa
Taifa
kwa madai kuwa, kipindi hiki ukarabati wa uwanja huo sehemu ya pitch
imeonekana fuvu la kichwa cha mtu, taarifa ambazo zimesambaa sana katika
mitandao ya kijamii.

Alex Nkenyenge

Pitch ya uwanja wa Taifa ikiendelea na ukarabati wa upandaji wa nyasi mpya
“Kwanza hiyo ni taarifa ya uongo na
hakuna fuvu isipokuwa ni madude ambayo yamepatikana kwenye mchanga
baada ya kuwa tumefukua sehemu ya uwanja, kwa hiyo hakuna kitu
kinachoitwa fuvu la mtu wala nini ni madude tu yaani mamimea yale
yaliyooza basi yanafanana kama magimbi ambapo ndani lilikuwa
limeshaliwa” Alex Nkenyenge
“Sasa kwa sababu mtu analiona kwa mbali anasema fuvu sasa
sijui fuvu litakujaje hapa, kwanza kilichotokea hilo dude limekuja na
mchanga wala halikuwa ndani ya uwanja, yaani kwenye mchanga uliyoletwa
ambao tulikuwa tunajaza kwenye pitch baada ya kuwa tumeondoa lea ya juu” Alex Nkenyenge

Kilichokuwa kinadaiwa kuwa fuvu
“Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho
bahati mbaya kwa watanzania wanapenda kuzungumza vitu vibaya kuliko
vizuri, maana mtu haulizi wala kushangaa ile inayosafisha uwanja, sasa
kama ni fuvu unataka kusema uwanja wa Taifa kulikuwa na makaburi?” Alex Nkenyenge
No comments:
Post a Comment