UTAFITI: Madhara ya kuendesha gari kwa muda mrefu usiyoyafahamu
Kwa mujibu wa Watafiti hao ni kwamba matokeo ya utafiti huo yanaweza kuelezewa kwa hoja kwamba ubongo hufanya kazi chini ya kiwango wakati wa safari ndefu.
Project hiyo ilishuhudia zaidi ya nusu milioni ya wakazi wa Briton wenye umri wa kati ya miaka 37 na 73 kufanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka mitano huku watu 93,000 kati yao wakikiri kuendesha gari kwa zaidi ya saa mbili kwa siku ambapo Watafiti wamebaini sio tu kuwa husababisha kudhoofisha nguvu za ubongo lakini pia kiwango cha IQ hupungua haraka ukilinganisha na ambao hawatumii muda mrefu wakati wakiendesha.
Dr. Kishan Bakrania, kutoka University of Leicester, aliiambia The Sunday Times:>>>”Tunajua kwamba kuendesha gari kwa zaidi ya saa mbili au tatu kwa siku ni mbaya kwa moyo wako. Utafiti huu unaeleza ni hatari kwa ubongo wako pia, huenda kwa sababu hufanya kazi chini ya kiwango katika saa hizo.”
No comments:
Post a Comment