Ali Kiba amsainisha Ommy Dimpoz RockStar4000
Siku chache baada ya Ali Kiba kuchaguliwa kuwa mmoja kati ya wamiliki
na wakurugenzi wa kampuni ya muziki Afrika ya Rockstar4000 na Rockstar
TV, leo ameanza kazi kwa kasi kumsainisha mkataba Ommy Dimpoz.
Ommy Dimpoz ambaye ni bosi wa PKP, ameweka wazi taarifa za kusaini
mkataba huo na kuwa mwanafamilia rasmi wa Rockstar4000, leo kupitia
akaunti yake ya Instagram.
”My fans! its official, I’ve signed with the biggest music company in
Africa *RockStar4000 as my new manegementteam and with the premiere Pan
Africa Music Entertainment content & News Channel,” ameandika Ommy
Dimpoz.
Hili ni shavu lingine zito kwa Ommy Dimpoz kutoka kwa King Kiba baada
ya kumsaidia kumtambulisha kwa nguvu kwenye mkondo mkuu wa muziki wa
Bongo Fleva kwa ngoma yake iliyomtambulisha ‘NaiNai’.
No comments:
Post a Comment