Wema Sepetu awaonya wajawazito kupiga picha za utupu
Aliyekuwa Miss Tanzania 2006, ambaye kwa sasa ni muigizaji wa Bongo
movie, Wema Sepetu amewatolea uvivu wanawake wote wenye mimba wanaopiga
picha za utupu kuonesha matumbo yao wakiwa wajawazito.
Wema Sepetu amewapaka wanawake hao na kusema kuwa waache kuweka picha za matumbo yao yenye mistari ya ujauzito.
”Muache kutuwekea mipicha ya mitumbo yenu yenye mstari ya ujauzito” ameandika Wema Sepetu kupitia ukarasa wake wa Instagram.Hata
hivyo mrembo huyo hakutaka kuwaacha salama wanawake wenye tabia hiyo,
amewaonya kuacha kuiga tamaduni za kizungu na kutakiwa kudumisha na
kuzienzi tamaduni zao za kiafrika zinazowataka kujistili.
Aidha ya yote Wema Sepetu alianza kwa kujikubali kuwa yeye kuwa sio
mwanamke wa kwanza kutojaaliwa mtoto, lakini sio sababu ya yeye kuacha
kusema ukweli pale anapoona mambo hayaendi sawa.
Wema alichukua nafasi hiyo kumpongeza Esha Buheti kwa kuwa tofauti na
wanawake wengine baada ya kuposti picha yake akiwa mjamzito huku
amejistili.
No comments:
Post a Comment