Ridhiwani amuonya Dr. Kigwangalla kuwa anaweza kuwa sehemu ya Uchochezi
Aliweka picha ya vijana wa Kitanzania wakionekana kupambania kupata kazi TRA ambapo iliripotiwa kwamba nafasi za kazi zilizotangazwa na TRA ni 400 lakini waliojitokeza ni zaidi ya elfu 30.
Sasa baada ya kuiweka hiyi picha Dr. Kigwangalla aliandika “Je, hii inaashiria ukubwa wa tatizo la ajira nchini ama ni kwamba watu wetu wanachagua sana kazi za kwenda? #NjeyaBox”
Baada ya picha hiyo kupostiwa kwenye Twitter ya Dr. Kigwangalla baadhi ya Watanzania walitoa maoni yao ambapo miongoni mwao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aliemuandikia >>> “Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakua sehemu ya wachochezi! Mh. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lkn picha inatoa jibu sahihi”
No comments:
Post a Comment