Ommy Dimpoz awajibu wanaosema anajipendekeza kwa Matajiri
Moja ya story ambazo zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao mbalimbali ni kuhusu Ommy Dimpoz kuitwa
chawa akidaiwa kuwaganda baadhi ya watu wenye uwezo kifedha wakifurahi
kitu ambacho amekanusha akisema watu wamekuwa wakijadili picha bila
kujua ukweli.
leo July 6, 2017 Ommy Dimpoz
amefunguka baada ya kuulizwa na Mtangazaji kuwa anadaiwa kupiga picha
na matajiri akiwa nao pamoja na kuishi maisha ambayo ni expensive.
>>>“Kwenye
kujipiga picha inahitaji umakini mkubwa sana kwa sababu picha unazopiga
zinaenda mbali sana. Huwezi kuamini sana safari yangu ya IBIZA nilikuwa
kwenye show Malindi Kenya mwaliko niliupata toka kwa shabiki yangu.
Shakaji aliyenipeleka IBIZA nilimueleza kuhusu mipango yangu ya kazi
akani-support katika video yangu ya Kajiandae.
“Nilipokwenda Dubai
nilitumia Hashtag ya Hello Dubai nikapata dili Dubai la kutangaza Utalii
wa Dubai. Watu wa Utalii wa Dubai walinilipa mkwanja kuweka picha
nikiwa Dubai, wakanipa offer ya video pia.” – Ommy Dimpoz.
Pamoja na taarifa hiyo habari nyingne inayotrend kutoka kwa staa huyo ni kusaini mkataba na Kampuni kubwa ya muziki ya RockStar4000 ambayo pia Alikiba amesainiwa.
No comments:
Post a Comment