Kalapina kuhusu kubadilika na kuwa Mwanaharakati wa Dawa za Kulevya
MuroTV
Burudani
Kalapina kuhusu kubadilika na kuwa Mwanaharakati wa Dawa za Kulevya
Kalapina amesema kufuatwa na Polisi kulimsaidia kubadilika lakini akidai hajutii kwa kuwa anachukulia kama sehemu ya maisha yaliyomkomaza na kumfanya kama alivyo sasa ambapo amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia vijana hasa walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.
>>>“Matukio mengine yalikuwa ya kufikirika kwetu sisi. Washikaji wa Kikosi cha Mizinga hatukuwa tukiyafanya kweli. Nakumbuka kipindi kile niliwahi kufuatwa na Polisi na Defender kama tatu hivi asubuhi naambiwa kuna wameibiwa mimi ni muhusika.
“Kama nisingebadilika nisingepata kura hata moja kwenye chaguzi zilizopita. Leo nimekuwa mtu wa kubadili maisha ya wengine.
Mbali na hayo Kalapina pia ameelezea tukio la kutekwa kwa Rapper Roma Mkatoliki akisema kama angelikuwa yeye siku hiyo angelipambana na watekaji hao na wangelimteka akiwa maiti.
>>>”Kama mimi wangekuja kuniteka kwanza wangenichukua maiti lakini wawili watatu wangekuwa wamelala chali. Sisi wakongwe hatuamini kabisa kwenye kiki maana kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. Ukweli tulikuwa hatupendi mambo ya ovyo.” – Kalapina

No comments:
Post a Comment