WENGER: SITOSAHAU HUJUMA NILIZOPATA MSIMU HUU
MuroTv
MICHEZO
Wenger: Sitosahau hujuma nilizopata msimu huu
Mkufunzi wa Arsenal ametaja ukosoaji ambao amekuwa akipata msimu huu kuwa hujuma ambayo hatosahau. Raia
huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 amekabaliwa na shutuma kali
kutoka kwa mashabiki kwa kumtaka kuondoka katika klabu hiyo ambayo
ameingoza tangu 1996.
''Sijali ukosoaji kwa sababu tunafanya kazi
ya umma'', aliambia BBC kabla ya mechi ya fainali kati ya Arsenal na
Chelsea katika uwanja wa Wembley.''Ninaamini kuna tofauti kati ya kukosolewa na kuchukuliwa hali ambayo hairuhusu kwa mwanadamu''.

''Klabu kilichoimarika ni kile kinafanya maamuzi .
Ni makosa kwamba katika kizazi kipya sio swali la iwapo uamuzi ni sawa lakini iwapo ni maarufu.Hilo halifai kufananishwa na uwezo wa mtu.Watu wenye majukumu lazima wafanye uamuzi wa sawa''.
No comments:
Post a Comment