MuroTv
MICHEZO
Mkenya ashinda mbio licha ya kupoteza kiatu

Mkenya Celliphine Chespol
alijizatiti baada ya kupoteza kiatu chake kwa muda na kuweka muda wa
pili bora katika historia ili kuweza kushinda mbio za mita 3000 kuruka
maji na viunzi katika mashindano ya riadha ya almasi ya Prefontaine
Classic Diamond League. Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 18
aliweka muda wa dakika 18 sekunde 58.57 licha ya kuvaa vizuri kiatu
chake cha mguu wa kulia katika raundi ya mwisho.Beatrice Chepkoech alikuwa wa pili huku Ruth Jebet anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio hizo akimaliza wa tatu
Kwengineko,
mwanariadha wa Ethiopia Genzebe Dibaba alishindwa kuvunja rekodi ya
dadake Tirunesh Dibaba katika mbio za mita 5,000.
Bingwa huyo
mwenye umri wa miaka 26 alishinda mjini Eugene Oregon kwa dakika 14 na
sekunde 25.22 ikiwa ni sekunde 14 nyuma ya muda uliowekwa na dadaake
2008.
No comments:
Post a Comment