Header Ads

SERIKALI KULIPA DENI LOTE LA UMEME

MuroTv

Serikali kulipa deni lote la umeme

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar italipa deni lote la umeme inalodaiwa na Shirika la Umeme (Tanesco) katika miaka miwili.
Waziri wa Ardhi, Nishati na Mazingira, Salama Aboud Talib, alisema hayo wakati akijibu swali la mwakilishi wa Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyeuliza kiasi cha deni. Alisema Zanzibar inadaiwa na Tanesco Sh bilioni 57.7 baada ya kupunguza deni hilo hivi karibuni kwa kulipa Sh bilioni 10.
Alisema deni hilo limeshindwa kulipwa kwa wakati kwa sababu mbalimbali ikiwemo Zanzibar kuongezewa kodi ya kununua umeme bila ya taarifa ya Tanesco. Alisema SMZ imeweka mikakati ili deni hilo lilipwe katika miaka miwili kuanzia sasa.
Alisema kasoro za kutoelewana kati ya Tanesco na Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco) zimepatiwa ufumbuzi wa kudumu. Hivi karibuni, Tanesco ilitishia kuikatia umeme Zanzibar kutokana na malimbikizo makubwa ya madeni ya muda mrefu.

No comments:

Powered by Blogger.