Header Ads

NDUGAI AIPONGEZA UDA-RT

 MuroTv

Ndugai aipongeza UDA-RT

31 Mai 2017
Spika wa Bunge, Job Ndugai
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema anatamani mabasi ya mwendo kasi yanayotoa huduma kwa sasa jijini Dar es Salaam, huduma zake pia zifike na kutoa huduma hizo mjini Dodoma.
Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa (CCM) pia aliishauri Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDART), kuboresha huduma zake kwa kuweka mabasi ya kutosha yanayokwenda kwa muda kama zinavyofanya nchi zilizoendelea.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake bungeni Dodoma jana, wakati akiipongeza kampuni ya UDA-RT kwa kuwa kampuni ya kwanza ya kizalendo kutoa huduma muhimu kama hiyo ya usafiri kwa mafanikio na kutimiza mwaka mmoja.
“Niwaambie tu Dodoma ndio mji mkuu hivyo pia mfikirie kuileta huduma hii huku kwa kuwa mji huu itafika mahala utahitaji UDA-RT. Mimi naamini iko kila sababu ya kuboresha huduma ya usafiri pia hapa Dodoma,” alisema.
Hata hivyo, aliishauri kampuni hiyo ya UDA-RT kuboresha zaidi huduma zake na kuongeza mabasi ya kisasa ili iweze kutoa huduma kwa kuzingatia muda na kuepuka kuwaweka wateja wake muda mrefu vituoni kama ambavyo nchi nyingi zilizoendelea zinavyofanya.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari wa UDA-RT, Joe Beda alisema watafanya kila linalowezekana kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu kwa kuwa ni moja ya miradi ya aina yake barani Afrika.

No comments:

Powered by Blogger.