utapeli unaotumika na mafundi wa Arusha Kuwaibia wajenzi
MuroTV
ARUSHA
utapeli unaotumika na mafundi wa Arusha Kuwaibia wajenzi
Kwa watanzania wote wajengao,kuna mchezo mchafu unaofanyika katika
viwanda vya mabati au wakala wao ambapo wauzaji na mafundi hushirikiana
kwa pamoja kumwibia mteja kwa mbinu hii…, fundi anapopima vipimo vya
mabati huwa wanakuwa na vipimo halisi (halali)na vingine
feki(alizoongeza kwa kila pc ya bati) mara nyingi huongeza nusu
mita(sentimita 50 hadi 70) hivyo anapokwenda kufanya manunuzi au kutoa
oda kwenye viwanda ama wakala wa kiwanda huwa na karatasi mbili, ile
feki yenye vipimo vilivyoongezwa ndio humpatia mwenye nyumba ambapo mara
nyingi mafundi hao huwa wameshaongea na wahusika ktk katika kiwanda au
wakala na humlazimisha mwenye nyumba kufanya manunuzi mahali
alipokusudia kufanya uhalifu huo(uwizi)hivyo vipimo vilivyoongwezwa mita
ndio hupigiwa mahesabu.
Mfano kwenye oda anapigiwa mahesabu ya mita 560 mara bei
waliyopatana,hivyo mteja hulipia mita 560,baada ya mteja kuondoka,fundi
huleta vipimo halisi. Mfano ni 480,hivyo ile tofauti basi hupigiwa
hesabu mara bei na kugawana fedha hizo, ambapo kwakweli ukiangalia
tofauti huwa ni kubwa sana huwa ni kati ya mita 70 hadi mita 120
kulingana na ukubwa wa nyumba,na bei kwa mita mara nyingi ni kati ya
12000 kwa mita hadi 11500 kwa mita.
Hivyo ukizidisha mara hizo mita,hujikuta fedha unazopoteza ni gharama za kumlipa fundi.
USHAURI: Kila mwenye kujenga ama mwenye kununua mabati haswa haya ya
kukatwa kwa mita, hakikisha unakuwa na kopi ya vipimo ambayo fundi
amekupa na unapokwenda kuchukua bidhaa yako hakikisha unapima kila pc
kulingana na kopi uliyonayo. Hakikisha bati zisipigwe hadi uhakiki.
Tuma ujumbe huu kwa kila group umuokoe mtanzania mwenzako katika
ubadhirifu huu unaofanywa na mafundi wengi wa kupaua nyumba
wakishirikiana na wenye kuuza mabati kwa kisingizio eti "matajiri
wanatubana kwenye malipo"
No comments:
Post a Comment