TRUMP AMTETEA MKWE WAKE JERAD KUSHNER KUHUSU URUSI
Trump amtetea mkwe wake Jared Kushner kuhusu Urusi 
Image caption
Jared Kushner ni mmoja wa wasaidizi wakuu wa Donald Trump
Rais wa Marekani
Donald Trump amejitokeza kumtetea mkwe wake Jared Kushner, baada ya
taarifa kutokea kwamba Kushner, ambaye kwa sasa ni mshauri wake katika
ikulu ya White House, alijaribu kuanzisha njia ya kisiri ya mawasiliano
na maafisa wa Urusi.
Kwenye taarifa ambayo imekabidhiwa gazeti la New York Times, Bw Trump amemsifu Kushner na kusema kwamba anafanya "kazi nzuri".Hata hivyo, hajazungumzia moja kwa moja tuhuma zinazomkabili mwanamume huyo ambaye ni mumewe binti wa kwanza wa Bw Trump, Ivanka.
Taarifa zinadai kwamba Bw Kushner alijadiliana na balozi wa Urusi kuhusu uwezekano wa kuanzisha njia ya kisiri ya kuwasiliana na maafisa wa Urusi mwezi Desemba.
- Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri
- FBI wamchunguza mkwe wa Trump, Kushner
Anadaiwa kufanya hivyo kabla ya Bw Trump kuapishwa kuwa rais, na kwa hivyo wakati huo alikuwa tu raia wa kawaida.
Tuhuma hizo zimeibuka baada ya Bw Kushner kudaiwa kuwa miongoni mwa wanaochunguzwa na FBI kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016.
Taarifa nchini Marekani zinasema maafisa wana habari muhimu, lakini kwamba si lazima iwe kwamba hilo lilikuwa kosa la jinai.

Bw Trump, ambaye inadaiwa alikutana na mawakili White House siku ya Jumapili, ambaye bado anamuunga mkono Bw Kushner, ambaye kwa sasa ni mshauri wa ngazi ya juu White House.
"Jared anafanyia nchi hii kazi nzuri sana. Nina imani naye kikamilifu," alisema kupitia taarifa kwa New York Times.
"Anaheshimiwa na karibu kila mtu na anafanyia kazi mipango ambayo itasaidia nchi yetu kuokoa mabilioni ya dola. Kadhalika, na labda muhimu zaidi, yeye ni mtu mwema."
- Mkwe wa Trump alitaka kuzungumza na Urusi kwa siri
Waziri wa usalama wa ndani John Kelly aliwaambia waandishi wa habari Jumapili kwamba ni kawaida kuwa na njia za kisiri za kuwasiliana na mataifa yenye ushawishi.
Mshauri wa usalama wa taifa wa Bw Trump HR McMaster pia alisema "tuna njia za faragha za kuwasiliana na mataifa kadha."
No comments:
Post a Comment