Header Ads

VITUO VIPYA VYA POLISI 65 KUJENGWA

MuroTv

Vituo vipya vya polisi 65 kujengwa

31 Mai 2017
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuf Masauni
SERIKALI imepanga kujenga vituo vipya vya Polisi 65 nchi nzima. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alibainisha hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Shauri Moyo, Mattar Ali Salum (CCM).
Salum alitaka kujua ni lini serikali itaanza kujenga vituo vipya vya polisi na kukarabati vingine kisiwani Unguja. Masauni alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha wilaya mpya zote nchini zinakuwa na vituo vya polisi na zile zenye vituo vya zamani vitakaribatiwa.
Akijibu swali la msingi la Mbunge Salum aliyetaka kujua ni lini askari watajengewa nyumba bora ili nao wajisikia serikali yao inawajali, Masauni alisema ni kweli kwamba Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa nyumba za kuishi askari.
“Katika kukabiliana na tatizo hilo, serikali ina mpango wa kujenga nyumba 350 za kuishi askari Polisi Zanzibar ambapo nyumba 150 zitajengwa Pemba na nyumba 200 zitajengwa Unguja,” alisema. Alisema kipaumbele cha serikali kwa sasa ni kujenga nyumba mpya za kisasa na si kukarabati nyumba zilizoachwa na wakoloni.

No comments:

Powered by Blogger.