WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MIRADI WILAYA YA MBEYA MJINI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Methadone Clinic ambao ni maalum kwa kuwahudumia na kuwapa ushauri nasaha waathirika wa madawa ya kulevya kwenye . hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salim Jessa (wanne kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya wakati alipoembelea kiwanda hichi Julai 31, 2017. Watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salim Jessa (kulia) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya wakati alipoembelea kiwanda hicho Julai 31, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS- Pepsi kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya, Julai 31, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wakazi wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Ruanda Nzove jijini humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi
No comments:
Post a Comment