Header Ads

JAFO APONGEZA MSHIKAMANO WA VIONGOZI NA WATENDAJI RORYA

Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi na
watendaji wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Rorya kwa mahusiano
mazuri waliyonayo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Jafo alitoa sifa hizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na watumishi .

Katika
ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa,
mabweni, maabara, na vyoo kwa sekondari ya Nyamtinga na Nyamunga ambapo
majengo hayo yamebainika kujengwa kwa ubora wa kuridhisha. 

Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu zaidi ya sh.milioni 500 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchini
Kwa
upande wake,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Agness Marwa
amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kufika wilayani Rorya na kwamba
amekuwa Waziri pekee aliyefanikiwa kutembelea wilayani humo katika
kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano. 



Mbunge
huyo ameishukuru serikali kwa upendo wake wa kuisaidia wilaya hiyo
miradi ya maendeleo. Naibu Waziri Jafo leo amekamilisha ziara yake ya
kikazi ya siku sita ya kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na
watumishi kwa mkoa wa Kagera na Mara na anaendelea na ziara yake katika
mikoa mingine.

.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikata utepe na kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Nyamtinga wilayani Rorya. 
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyokaguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Mbunge wa Vitimaalum Agnes Marwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Rorya na kuwapongeza kwa ujenzi wa madarasa na mabweni.

No comments:

Powered by Blogger.