Header Ads

DC MNDEME AMPONGEZA MAVUNDE KWA KUTATUA KERO YA MAJI KWA WANANCHI WAKE

Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christine Mndeme leo amezindua mradi wa Maji
katika kijiji cha Mhande,Kata ya Ngh’ong’hona ambao umefadhiliwa na
Shirika shirika la wamishionari wa damu takatifu ya Yesu(CPPS)
uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 35.

Mradi huu umetokana na
maombi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa Shirika la
hilo kusaidia kutatua changamoto ya Maji katika kata hii ya
Ngh’ongh’ona ambayo wananchi wake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo kubwa
la upatikanaji maji safi na salama.

Akizungumza katika
uzinduzi huo, Mndeme amelishukuru shirika hilo la CPPS kwa ufadhili wa
mradi huo na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde
kwa kuwa mstari wa mbele kutatua kero za wanachi wake hususani kero
kubwa ya Maji katika kata ya Ngh’ongh’ona.

Amesema kutatuliwa kwa kero hiyo kumewatua kina mama ndoo kichwani kwa kuwa walikuwa wakienda kuchota maji umbali mrefu.


“Mwili unahitaji maji unapotafuta maji mbali roho inasononeka hata muda
wa kusali unaukosa, tunashukuru sana shirika hili lakini wananchi tuna
wajibu wa kuutunza mradi huu ambao ni wa thamani kubwa sana,”amesema
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada. 
Wananchi wa Mhande wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Chritine Mndeme katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kijiji hicho. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme pamoja na Father Fransis wakifungua bomba la maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji katika  kijiji cha Mhande. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akisalimiana na father Fransis .

No comments:

Powered by Blogger.