Header Ads

VIGOGO 3 FAIDIKA LTD MBARONI KWA WIZI WA FEDHA TSH. MILION 700 DAR

Na
Prosper Muro ✍

23 June 2021
Kisutu, Dar Es Salaam

Wafanyakazi watatu wa Taasisi ya fedha ya Letshego maarufu kama Faidika Limited, wamefikishwa katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la la wizi wa sh milioni 700.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Faraja Ngukah mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Elisha Tengeni , Donald Kwaya na Elisha Mboka.

Akisoma shitaka hilo, wakili Ngukah aludao alidai kati ya Januari mwaka 2016 hadi Septemba mwaka 2017 washitakiwa waliiba sh milioni 700 mali ya Kampuni ya Letshego Tanzania Limited maarufu kama Faidika fedha ambazo zilifika kwao kutokana na nafasi zao za uwajili.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao wasilisha mahakamani fedha taslim au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 350.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Juni 30 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wote wamepelekwa maabusu.

Tufuatilie Kwenye Kurasa Zetu Mbalimbali
Youtube: Muro Tv
https://youtube.com/channel/UCLhgLgldtWYfghAkFPpOw7Q

Facebook: Muro Tv
https://m.facebook.com/MuroTv/

Instagram: @murotvtv
https://www.instagram.com/murotvtz/

Twitter: @murotvtz
https://mobile.twitter.com/Murotvtz

No comments:

Powered by Blogger.