MAKAMU WA RAIS AZINDUA MPANGO MKAKATI WA WATER AID TANZANIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana leo amezindua Mpango Mkakati wa Water AID Tanzania .
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Mkurugenzi wa Water Aid Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Olutayo Bankole –Bolawole,Mkurugenzi WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole na wadau mbali mbali wa maji, afya na mazingira.
Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Water Aid Tanzania wenye lengo la “ Kuweka Maji Safi na Usafi wa Mazingira (WASH)” katika mipango ya Maendeleo ya Jamii.
Makamu wa Rais aliwapongeza Water Aid Tanzania kwa mpango wake huo, alisema Maji ni rasilimali ambayo haijawahi kutosheleza mahitaji ya dunia na hapa kwetu pia kwani kuna mahitaji makubwa ya maji kwa ajili ya shughuli za kijamii, kiuchumi na kuhuisha na kutunza mazingira.
Vilevile vyanzo vya maji vinaathiriwa sana na Ukame,kufurika n, kuvuruga mtiririko asilia, mabadiliko ya hali ya hewa ongezeko la idadi ya watu na viumbe wengine (Wanyama).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohamoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu maalumu chenye mpango mkakati wa Water Aid .
No comments:
Post a Comment