Marekani || Trump aapa kuujenga ukuta wa Mexico
Donald Trump amesema kuwa
atalizimika kuweka kando shughuli za serikali ikiwa itahitajika, ili
aweze kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico.
Trump aliwaambia wafuasi wake kwenye mkutano uliofanyika huko Phoenix, Arizona, kuwa wabunge wa Democrats ndio kizuizi.Wakati wa hotuba yake iliyochukua dakika 80, pia Trump alivilaumu vyombo vya hahari kwa kuwaunga mkono makundi yenye ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Trump anataka bunge la Congress kufadhili mpango wake wenye utata wa kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico ili kuwazuia wahamiaji haramu.
Lakini warepublican watahitaji uungwaji mkono wa Democrats ili kuweza kupata pesa za kujengwa ukuta huo.
Katika hotuba yake bwana Trump alisema kuwa Democrats wanaliweka taifa la Amerika hatarini.
Alisema kuwa maafisa wa uhamiaji wanaofanya kazi eneo hilo wanasema kuwa ni muhimu kuzuia wahamiaji haramu kuingia Marekani.
Huku hotuba ya Trump ikishangiliwa ndani ya ukumbi, wale wanaompinga Trump waliokuwa wamekusanyika nje ya mkutano huo walikabiliana na polisi baada ya mkutano huo kumalizika.
Polisi walilazimika kutumia maji ya kuwasha wakati waandamanaji walianza kurusha mawe na chupa.
No comments:
Post a Comment