Idadi ya watoto wanaotumiwa kama walipuaji wa kujitolea mhanga yaongezeka Nigeria
Kumekuwa na ongezeko kwa idadi ya
watoto wanaotuimiwa kama washambuliaji wa kujitolea mhanga na wanamgambo
wa Boko Haram, kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa Umoja wa
Mataifa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Unicef,
linasema kuwa tayari visa 83 vimeripotiwa mwaka huu, mara nne zaidi ya
vile vya mwaka wote wa 2016.55 kati yao walikuwa ni wasichana walio na umri chini ya miaka 15 na kwenye kisa kimoja, bomu lilifungwa kwa mtot ambaye alikuwa amebewa na msichana mdogo.
Unicef inasema mbinu hii imezua hofu kwa watoto wanaoachiliwa na Boko Haram.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto 127 wametumiwa kama walipuaji kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu mwaka 2014.
Wanamgambo wa Boko Haram mara kwa mara wamewatumia watoto, na wamewateka mamia ya wasichana wa shule na kuwalazimisha watoto wavulana kujiunga na jeshi lao.
No comments:
Post a Comment