Wizkid aendelea kupata mashavu kutoka mbele, safari hii ni Future
Milango ya neema inazidi kufunguka kwa Wizkid. Msanii huyo kutoka Nigeria amepata shavu la kuwa miongoni mwa wasanii watakao tumbuiza kwenye show za ziara ya rapper Future ‘The Future Hndrxx Tour’ kutoka Marekani.
Katika ziara hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kuwaka moto Julai 8 ya
mwaka huu, Wiz anatumbuiza katika show nne. Show ambazo Wizkid atawasha
moto ni pamoja na itakayo fanyika West Palm Beach, Atlantic City,
Syracuse na Uncasville (zote za nchini Marekani).
Kupitia mtandao wa Instagram, Wiz amethibitisha hilo kwa kuweka cover
ya show zake atakazofanya na kuandika, “Catch me on the road with
@future !! Bringing that African wave! #starboyworldwide #freebandz.”
Ziara hiyo ya Future itazunguka karibia nchi kibao duniani ikiwemo
kwenye bara la Marekani, Ulaya, Afrika na mengine. Ratiba hiyo pia
imeonyesha rapper huyo wa Marekani atatumbuiza katika jiji la Dar es
Salaam, kwenye viwanja vya Leaders Julai 22.
No comments:
Post a Comment