Taifa Stars wamepata nafasi ya mshindi wa tatu vs Lesotho
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo July 7 2017
imefanikiwa kuingia kwenye headlines baada ya kupata ushindi katika game
ya michuano ya COSAFA ya kutafuta mshindi wa tatu iliyochezwa Afrika
Kusini. Taifa Stars game ya kutafuta mshindi wa tatu imecheza dhidi ya
timu ya taifa ya Lesotho na dakika 90 zikamaliza kwa sare tasa (0-0)
kutokana na timu hizo kutoshana nguvu na kila moja kufanikiwa kumiliki
mpira kwa asilimia 50 ndio mikwaju ya penati ikaamua mshindi.
Licha ya Lesotho kuonekana kuwa wazuri kiasi na kufika golini kwa Taifa
Stars mara nyingi lakini hawakuwa wazuri katika upigaji penati na
wakajikuta wakifungwa kwa penati 4-2, huku kwa upande wa Tanzania Shiza
Kichuya ndio alikosa penati, Himid Maoa, Simon Msuva, Abdi Banda na
Raphael Alpha wakafunga penati zote.
No comments:
Post a Comment