BREAKING NEWS: MAJAMBAZI WA KIBITI SITA WAUWAWA NA POLISI, MWANZA
Na Muro Tv (Mwandishi Mr Muro)
Jeshi la polisi Mkoa wa mwanza limewauwa watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika mapigano yaliyodumu kwa masaa kadhaa usiku wa kuamkia Leo Juma mosi katika mtaa wa Fumajira kata ya Igoma
Jeshi la polisi Mkoa wa mwanza limewauwa watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika mapigano yaliyodumu kwa masaa kadhaa usiku wa kuamkia Leo Juma mosi katika mtaa wa Fumajira kata ya Igoma
Kamanda wa polisi Mkoa wa mwanza Ahmed Msangi amewaambia waandishi wa habari kuwa Polisi walifika eneo hilo mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu kikundi cha watu wanaopanga kufanya uhalifu
"Wiki tatu ama nne zilizopita tulipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna watu wawili-watatu wameingia kutoka Mkoa wa Pwani-Kibiti kule ambapo operation wa kusaka wauwaji inaendelea na wamefika hapa na kuanza kujikusanya na kutaka kufanya mauaji kama yale yanayotokea kule KIBITI pamoja na kufanya unyanganyi wa kutumia silaha pamoja na kuuwa watu, kutokana na taarifa hizo ilibidi tuanze kufanya upelelezi wa uhakika na kwa kina na kuweza kumkamata.....mtu mmoja ambae jina siwezi kumtaja ee tulimkamata.....siku sita zilizopita, na katika mahojiano aliweza kutusaidia kwasababu ee alishirikiana vizuri....kutueleza hilo kundi ambalo walishaanza kujioganize.......na zaidi akaenda mbali zaidi na kusema kuwa walishafanya tukio moja kwenye moja ya Bekery ambayo ipo hapa Mwanza, hiyo Bekery inaitwa Victotia Bekery " Alisema kamanda Ahmed Msangi
Amesema baada ya kuwazingira Majambazi hao walianza kuwamiminia Risasi na Polisi kujibu mapigo na kuwauwa watu sita waliokuwa kwenye Nyumba hiyo...
Wamesema baada ya kuingia kwenye nyumba hiyo na kuwafanya upekuzi wamekuta baadhi ya vifaa vya kijeshi zikiwemo Sare, Silaha na Risasi
"Silaha mojawapo ni AK 47 na Magazine ambayo imejaa Risasi......hizi ni Unifomu lakini ukiziangalia unifomu hizi zinaonekata ni za kijeshi lakini Jeshi letu halitumii Unifomu za aina hii......na hichi ni kitambaa cha kutanda kichwani" Alisema Kamanda Ahmed Msangi
Hata hivyo watu wawili waliokimbia katika nyumba hiyo bado juhudi za kuwasaka zinaendelea
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesisitiza umuhimu wa Serikali za mitaa kusajili wageni wote wanaoingia katika maeneo yao na yeyote atakaekaidi amri hiyo achukuliwe hatua kali
"Yeyote katika ngazi yake ambaye atafanya uzembe katika hili atawajibika....hatutoshi tukishakuwa wote tunahangaika na vita hii tukatuta ofisi ya mtendaji na mtaa hawana Ledger ya wageni...hawana ledger wa wakaazi unamsaidiaje huyu? zaidi ya kumtoa...ndio dawa yake tu na inawezekana anataka kutoka anatafuta sababu tu anashindwa kusema anasubiri tumfumanie pale tumtoe.... sisi tutamsaidia kumtoa" Alisema Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela
Pia kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Fumagira...Bulugu Kitambo amesema kati ya watu sita waliouwawa wamemtambua mtu mmoja ambae anasemekana alekuwa ni fundi bodaboda.
ANGALIA VIDOE HAPA CHINI
-----Endelea kukaa karibu na Muro TV kwa mengi zaidi-----
No comments:
Post a Comment