Header Ads

Mshahara anaohitaji Alex Sanchez ili asaini mkataba mpya Arsenal

 
Siku moja baada ya club ya Arsenal kutangaza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea Olympique Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette, leo July 6 mshambuliaji wa Arsenal raia wa Chile Alex Sanchez ameripotiwa kutaja mapendekezo yake ili asaini mkataba mpya.
Sanchez ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2014 akitokea FC Barcelona ya Hispania, ametajwa kudai alipwe mshahara wa pound 400000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1.1 ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Arsenal.

Inaripotiwa kuwa Arsenal wapo tayari kumlipa Sanchez zaidi ya pound 275000 ambazo inaripotiwa ameahidiwa na Man City wakati FC Bayern Munich ambao wanamuhitaji wanasitasita kutoa ofa ya kiasi hicho cha mshahara licha ya kuonesha dhamira ya wazi ya kuhitaji huduma yake.
CHANZO: Daily mirror

No comments:

Powered by Blogger.