Kutoka Morocco Msuva alichoambiwa na kocha baada ya game
Winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Simon Msuva aliyekuwa anaichezea Yanga, Jumapili ya July 30 ikiwa ni siku nne zimepita toka asaini mkataba na timu ya Difaa El Jadid ya Morocco, ambapo ni mafanikio kutoka kucheza Tanzania nchi iliyopo nafasi ya 114 katika viwango vya FIFA anakwenda kucheza nchi iliyopo nafasi ya 60.
July 30 amepata nafasi ya kuichezea timu yake ya Jadid mchezo wa kwanza wa kirafiki na kufunga goli wakipoteza kwa magoli 2-1, kocha wa Jadid alimpanga Simon Msuva dakika 45 za pili licha ya kupoteza mchezo huo Msuva ndio alifunga goli la kufutia machozi kwa upande wa Difaa El Jadid.
“Nashukuru Mungu nimecheza
game yangu ya kwanza ya kirafiki na timu ya huku ipo daraja la kwanza,
dakika 45 za pili nikaingia lakini mwalimu aliniuliza maswali na
kuniambia ananichezesha namba 10 kwa sababu mimi nafunga haoni haja ya
kunichezesha winga.” – Msuva.
No comments:
Post a Comment