“Naomba tuheshimiane” Pochettino achoshwa na kelele za Conte na Mourinho
Kwa nyakati tofauti makocha wa Chelsea na Manchester United
wamekuwa wakiizungumzia Tottenham Hotspur na wachezaji wao suala ambalo
linaonekana kumkera sana kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino.
Pochettino hapendezwi na suala la makocha hao kupenda kuizungumzia
timu yake mara kwa mara huku wao Tottenham hawajawahi kuzizungumzia timu
hizo.
Conte amesema wiki hii anatamani kumnunua Kane na kueleza matarajio
ya Tottenham Hostpur huku Mourinho akisema Tottenham wana wakati mzuri
sana kwani wamemuuza Kyle Walker tu hadi sasa tofauti na matarajio ya
wengi.
“Mimi ni kocha ambaye sipendi hata kidogo kuzungumzia timu za
wenzangu wala makocha wenzangu hiyo inatokana na kwa sababu nina heshima
na naomba hata hao wenzangu waheshimu tunachofanya” alisema Pochettino.
Pochettino anaamini timu nyingine zina presha kubwa kwa sasa
“wametumia pesa nyingi katika usajili ni lazima wako katika presha kubwa
sana tofauti na sisi, sisi tuko vile vile vya siku zote hatuna cha
kupoteza” aliongezea Pochettino.
Pochettino pia amesisitiza Eric Dier hataenda popote. Tottenham
wamekuwa wakiwapa presha kubwa sana vigogo wa EPL katika siku za
karibuni hali inayopelekea wao kutazamwa kama tatizo kwa vilabu
vinavyotaka ubingwa.
No comments:
Post a Comment