Header Ads

UEFA imeipiga faini Man United na kumfungia mchezaji wao

 
Baada ya kupita siku kadhaa toka beki wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea Man United Eric Baily kufungiwa michezo mitatu na chama cha soka barani Ulaya UEFA, leo July 31 2017 UEFA limetangaza kumfungia mchezaji mwingine wa Man United.
UEFA leo imetangaza kumfungia Phil Jones mechi mbili kutokana na kupuuzia maafisa wa UEFA waliyotaka kumpima utumiaji wa dawa zisizoruhusiwa michezoni na kuendelea kufurahia ubingwa wa Europa, hata hivyo Phil Jones na Daley Blind wamepigwa faini ya pound 4500 kushindwa kufanya vipimo.
Phil Jones
Adhabu ya UEFA haijaishia kwa Phil Jones na Daley Blind bali kwa club pia ya Man United imepigwa faini ya pound 8,900 kwa kuvunja sheria kwa kushindwa kuhakikisha wachezaji wake wanapima, hata hivyo UEFA imewapa Man United siku tatu za kukata rufaa na inaendelea kumkosa Eric Baily aliyefungiwa mechi tatu.

No comments:

Powered by Blogger.