Header Ads

Aliyeshambulia kwa risasi nyumba ya Makamu wa Rais nchini Kenya auawa

Polisi nchini Kenya wamefanikiwa kumuua kwa kumpiga risasi mshambuliaji ambaye aliingia kwa nguvu nyumbani kwa Makamu wa Rais nchini Kenya, William Ruto.

Bwana Ruto na familia yaka hawakuwepo nyumbani wakati mtu huyo alivyoingia kushambulia nyumba hiyo iliyopo katika mji wa Eldoret.
Mwanamume huyo aliingia kwenye nyumba hiyo na kumjeruhi mlinzi wa mlango kwa upanga na kumnyanganya bunduki yake kabla ya kutekeleza mauaji ya mlinzi huyo.
Ripoti za awali zilisema kuwa watu kadhaa waliokuwa wamejihami waliingia nyumbani mwa Ruto lakini baadae polisi wakasema kuwa alikuwa ni mshambuliaji mmoja tu.

No comments:

Powered by Blogger.