ZIFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM
MuroTV
KITAIFA
ZIFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM

Umaarufu wa Dar es Salaam kwenye
shughuli za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu
kuvizingatia vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa
kuviona tu lakini bila ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana
na wageni huja wakitokea nchi mbalimbali kujifunza.
Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach
unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi eneo la Oyster Bay, Jumia
Travel ingependa kukufahamisha kwamba unaweza kujifunza na kufurahia
mambo mengi pindi utakapotembelea maeneo yafuatayo.
Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya
Utamaduni. Makumbusho haya awali yalifunguliwa mwaka 1940 kama
kumbukumbu ya Mfalme George wa tano ambapo kihistoria huwarudisha
watanzania nyuma walipotokea. Makumbusho haya huonyesha mabaki muhimu ya
binadamu wa kale yaliyogunduliwa na Dkt. Leakey aliyoyachimbua kwenye
bonde la Olduvai. Wageni wanaweza kujifunza urithi wa kitamaduni kutoka
kwa makabila mbalimbali Tanzania pamoja na athari za biashara ya utumwa
kipindi cha utawala wa kikoloni. Baadhi ya vitu vingine vinavyopatikana
katika makumbusho haya yaliyopo mtaa wa Shaaban Roberts ni zana za jadi,
desturi, mapambo na vyombo vya muziki.
Kijiji cha Makumbusho. Takribani
maili 6 kutokea katikati ya jiji, kuna kiji cha makumbusho ambacho
kimehifadhi tamaduni za makabila zaidi ya 120 yanayopatikana Tanzania.
Wageni wanaweza kuzunguka kwenye vibanda kadhaa vya nyasi
vinavyopatikana pale kwenye ukbwa wa takribani hekari 15 na kujionea
ufundi wa kijadi katika kuchora, ufumaji na uchongaji. Kijiji hiki
kinachopatikana eneo la Kijitonyama, barabara ya Bagamoyo pia huwa na
ngoma na michezo ya jadi pamoja shughuli nyingize za kitamaduni.
Sanamu la Askari; Likiwa
limetengenezwa kwa shaba sanamu hili ya Askari huonyesha askari akiwa
amevalia vazi rasmi lililotumika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia
huku ncha ya mbele ya bunduki (kama kisu) ikiwa imeelekezwa karibu na
bandari iliyopo jirani. Sanamu hili huonyesha kama kumbukumbu ya majeshi
ya waafrika walioshiriki kupigana kwenye vita ya Kwanza ya Dunia na
linapatikana mtaa wa Azikiwe na Samora.

Boma la Kale; Likiwa limejengwa
mnamo mwaka 1866 mpaka 1867 na Majid Bin Said, Sultani wa Zanzibar, Boma
hili la kale ni jengo lenye umri zaidi ambalo linapatikana kwa sasa
jijini Dar es Salaam. Jengo hili lilitumika kuwakarabisha wageni wa
Sultani ambaye alikuwa na kasri lake pembeni yake. Vitu vya kuvutia
kwenye jengo hili lililopo mtaa wa barabara ya Sokoine ni namna
lilivyojengwa kwa ndani vikiwemo mlango wa mbao kutokea Zanzibar na kuta
zilizojengwa kutokana na matumbawe.
Muro Tv Ipo Play Store…Download HAPA ,Tuwe tunakutumia habari kwa haraka zaidi,kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba:0768786851, whatsapp:0768786851
No comments:
Post a Comment