Je wajua noti zilianza kutumika rasmi mwaka 1905 Tanzania Bara? Ijue Historia ya Sarafu na Noti za Tanzania
Kwa muda mrefu fedha zilizotumika katika nchi hii zilikuwa ni sarafu. Noti za karatasi zilianza kutumika mwaka 1905 wakati wa utawala wa mjerumani kwa upande wa bara. Noti hizo zilitolewa katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na rupie 500 kama ionekanavyo hapa chini. Noti za rupie 500 zilikuwa chache sana na sikufanikiwa kupata picha yake
Rupie 5
Rupie 10
Rupie 50
Rupie 100
Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo wa 1905, noti za Rupee za kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee 5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata picha zake zote, naonyesha mfano wa noti za rupee 5 tano tu niliyofanikiwa kupata.
5 Zanzibari rupee
Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, serikali ya kijerumani ilitoa noti za
dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi
zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa
hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana na sikufanikiwa kupata picha yake
1 Rupie
5 Rupien
10 Rupien
20 Rupien
50 Rupien
Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.
Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili kwa dar es
salaama wakati wa serikali ya kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika
Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa
inaitwa "Tabora Pound."
.....INAENDELEA
No comments:
Post a Comment