WATU 30 WAHUKUMIWA KIFO KIFO MISRI KWA MAUAJI YA MWENDESHA MASHTAKA
MuroTV
WATU 30 WAHUKUMIWA KIFO KIFO MISRI KWA MAUAJI YA MWENDESHA MASHTAKA

Hisham Barakat alikufa kwenye shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari miaka miwili iliyopita.
Alikuwa miongoni mwa maafisa waandamizi wakuu kuuawa na wanamgambo katika miaka ya karibuni.
Bwana Barakati alihusishwa na maelfu ya kesi ya wapiganaji wa Kiislamu kufuatia mapinduzi ya serikali ya Misri iliyokuwa ikiongozwa na Muslim Brotherhood.
Mamlaka za dini za nchi hiyo sasa wataamua iwapo waidhinishe hukumu ya vifo iliyopitishwa na mahakama.
Misri iliwalaumu kundi la Musclim Brotherhood na lile la Gaza la Hamas kwa mauaji ya Bwana Barakat licha ya makundi yote mawili kukana kuhusika.
Mwaka uliopita wizara ya mambo ya ndani ilitoa video ikionyesha wanaume kadha wakikiri kuhusika kwenye mauaji hayo na kusema kuwa walienda huko Gaza kupata mafunzo kutoka kundi la Hamas.
Baadaye baadhi yao walikana madai hayo mahakamani wakisema kuwa walikuwa wameteswa ili kukiri
Muro Tv Ipo Play Store…Download HAPA ,Tuwe tunakutumia habari kwa haraka zaidi,kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba:0768786851, whatsapp:0768786851

No comments:
Post a Comment