MELI YA JESHI LA MAREKANI YAGONGONA NA YA MIZIGO,WANAJESHI 7 HAWAJULIKANI WALIKO
MuroTV
MELI YA JESHI LA MAREKANI YAGONGONA NA YA MIZIGO,WANAJESHI 7 HAWAJULIKANI WALIKO
Wanajeshi
saba wanamaji wa Marekani hawajulikani waliko baada ya meli yao USS
Fitzgerald, kugongana na meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya
Ufilipino, katika pwani ya mashariki mwa Japan.
Walinzi wa pwani ya Japan wametuma maboti matano na ndege mbili katika eneo hilo kusaidia katika shughuli za uokoaji.
Msemaji wa jeshi la maji la Marekani, amesema huenda maafisa hao wako sehemu za ndani za zilizofungwa ili kuzuia maji zaidi kuingia ndani ya manuari hiyo.

Meli ya ACX Crystal iliontkana kugeuka kabl aya jali hiyo kabla ya kuelekea mjini Tokyo
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya meli ya pili iliyokuwa na bendera ya Ufilipino ACX Crystal.
Meli ya Japan kuisindikiza meli ya Marekani
Kati ya waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa njia ya helikopta
Kati ya waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa njia ya helikopta

Uharibifu kwenye meli ya mizigo ya ACX
Meli hiyo ya kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa Yokosuka.
Meli ya kijasusi ya Urusi yazama Uturuki
Picha zilionyesha uharibifu mkubwa kwenye meli ya kijeshi baada ya ajali hiyo.
Waliojeruhiwa wakiondolewa kutoka meli ya Japan
Haijulikani ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa ikielekea wakati huo.

Ndege za kuangusha mabomu za Marekani zapaa Korea
Meli ya mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan ya Nagoya na Tokyo.

Meli ya mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan ya Nagoya na Tokyo.

Muro Tv Ipo Play Store…Download HAPA ,Tuwe tunakutumia habari kwa haraka zaidi,kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba:0768786851, whatsapp:0768786851

No comments:
Post a Comment