Ripoti ya Prof. Osoro yaichanganya ACACIA, yaipinga huku ikitangaza kupunguza wafanyakazi 400
MuroTv
KITAIFA
Ripoti ya Prof. Osoro yaichanganya ACACIA, yaipinga huku ikitangaza kupunguza wafanyakazi 400
n
Afisa Habari na Mahusiano ya Jamii wa Kampuni hiyo, Nectar Foya amesema kampuni hiyo inatarajia kuingia mkataba na kampuni binafsi ambayo itaendesha shughuli za ulinzi wa migodi yake, ikiwemo wa Bulyanhulu na Buzwagi.
“Tumeamua kuingia mkataba na kampuni ya ulinzi kwa sababu ndio njia pekee ya kulinda rasilimali zetu na kuzuia kuendelea kupata hasara,” amesema.
Katika hatua nyingine, kampuni hiyo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa Juni 12, 2017, inapinga ripoti ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Makinikia aliyokabidhiwa Rais John Magufuli mapema hii leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo Prof. Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ya Acacia inadai kuwa, matokeo ya uchunguzi wa kamati hiyo juu yake si ya kweli na kwamba hayaendani na uhalisia wa utendaji kazi wake hapa nchini kwa zaidi ya miaka ishirini.
FOLLOW NA LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK HAPA CHINI
CLICK HAPA ☛ OPEN
FOLLOW ACCOUNT YANGU YA INSTAGRAM
CLICK HAPA ➼ OPEN
MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;



No comments:
Post a Comment