Waziri Ndalichako akabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa
MuroTV
MATUKIO
Waziri Ndalichako akabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako
amewataka wanafunzi nchini kuwa na Nidhamu kwani bila nidhamu hakuna
mafanikio yanayoweza kupatikana.
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo hii leo mjini Dodoma wakati
akikabidhi tuzo na zawadi mbalibali kwa wanafunzi waliofanya vizuri
katika mitihani ya kumaliza shule ya msingi, kidato cha Nne na wale wa
kidato cha sita ambapo amewasisitiza wanafunzi wa kike kujiepusheni na
mapenzi wakati wakiwa mashuleni.
Waziri Ndalichako amewataka wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidii,
ambapo pia amewaonya wanaowanyemelea wanafunzi kwa lengo la kuwaharibia
masomo na ndoto walizonazo kuwa sheria ni kali na ikithibitika
muhusika atakwenda jela miaka 30.
Viongozi wengine walioambata na waziri katika shughuli hiyo ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo na
Naibu Katibu Mkuu Profesa Saimon Msanjila.
Kauli mbiu ya siku ya Elimu ni: Elimu ni nguzo muhimu kwa Maendeleo ya viwanda
Pia usisahau ku like page yangu ya facebook hapo chini ama kwa kunifuata Facebook Tafuta / search @ Muro Tv
FOLLOW NA LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK HAPA CHINI
CLICK HAPA ☛ OPEN
FOLLOW ACCOUNT YANGU YA INSTAGRAM
CLICK HAPA ➼ OPEN
MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;



No comments:
Post a Comment