UTAFITI: Unapotumia Instagram, Twitter, Facebook tambua unapata madhara haya…
MuroTV
fB insta twitter
UTAFITI: Unapotumia Instagram, Twitter, Facebook tambua unapata madhara haya…
Kwa mujibu wa Wanasaikolojia hao, miongoni mwa athari zinazosababishwa na Instagram pamoja na kusababisha magonjwa ya akili kama vile Bipolar, msongo wa mawazo uliopitiliza, kutamani kujiua, kukosa kujiamini na kuwa mpweke tofauti na mitandao mingine.

Katika utafiti uliofanywa kwa kuwahusisha zaidi ya 1,500 wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 24, zaidi ya watu 1,300 walitajwa kuathirika zaidi na mtandao huo ukilinganisha na mitandao mingine huku miongoni mwa sababu zilizotajwa kuongoza kwake ni pamoja na kuwa sehemu ya watu kutukanana na kuonesha maisha ya juu ambayo si halisi.
Aidha, utafiti umeonesha pia kuwa YouTube ina athari ndogo zaidi tofauti na mitandao mingine baadhi wakiutaja kama sehemu wanayopata furaha kwa kuangalia video zinazofundisha mambo mbalimbali.

MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;

No comments:
Post a Comment