KAMPUNI YA MAXCOM AFRIKA YATOA WITO KWA MAKAMPUNI NCHINI KUUZA MITAJI KATIKA SOKO LA HISA ILI KUKUZA UWEKEZAJI
MuroTV
MATUKIO
KAMPUNI YA MAXCOM AFRIKA YATOA WITO KWA MAKAMPUNI NCHINI KUUZA MITAJI KATIKA SOKO LA HISA ILI KUKUZA UWEKEZAJI
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max
Malipo) Dkt.Donalth Ulomi akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari
wakati wa kutambulisha hati itakayoiwezesha kampuni hiyo kuuza hisa
zake kwa umma Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max
Malipo) Dkt.Donalth Ulomi (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na
waandishi wa habari ambapo Kampuni hiyo ilitambulisha hati
itakayoiwezesha kuuza hisa zake kwa umma Jijini Dar es Salaam,
kushoto ni Mkurugenzi Msimamizi Bw.Ahemed Lussasi.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max
Malipo) Dkt.Donalth Ulomi(kushoto) na Mkurugenzi Msimamizi wa Kampuni
hiyo Bw.Ahemed Lussasi wakionyesha bango jipya la kampuni hiyo katika
mkutano wa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.(Picha na Mpiga
Picha wetu).
……………………
Na Mwandishi Wetu
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika (Max
Malipo) Dkt.Donalth Ulomi ametoa wito kwa makampuni nchini kuuza mitaji
yao katika soko la Hisa ili kutimiza adhama ya Serikali ya kupanua wigo
wa umiliki wa makampuni.
Dkt.Ulomi aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano
na waandishi wa habari ambapo Kampuni hiyo ilipata fursa ya
kutambulisha hati itakayoiwezesha Maxcom kuuza hisa zake kwa umma.
“Leo kampuni yetu imetoa hati rasmi inayotambulisha Maxcom Afrika
kuwa moja ya kampuni inayomilikiwa na umma, ambapo ni hatua nzuri kwetu
na fursa kwa wananchi wa kitanzania kuwekeza kupitia manunuzi ya
hisa”alisema Dkt.Ulomi.
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa hatua hiyo ni katika kutekeleza
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli, ambapo ameyataka makampuni nchini kuuza asilimia 25 ya hisa
zake kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Dkt. Ulomi amezidi kufafanua kuwa kampuni hiyo ipo katika hatua za
kukamilisha mchakato wa kubadili jina na kuwa Maxcom Afrika Public
Limited Company (Maxcom Africa Plc) ambapo kwa sasa inangojea kibali
cha wasimamizi wa soko la hisa ili iaanze kuuza mara moja kwa watanzania
watakaokuwa tayari kuwekeza.
Maxcom Afrika PLC ni kampuni iliyoanzishwa na vijana wazawa wa
kitanzania na imefanikiwa kutoa ajira takribani 449 moja kwa moja kwa
zaidi ya watanzania elfu 16 huku ikiwa na lengo la kutoa ajira laki moja
ifikapo mwaka 2020.

No comments:
Post a Comment