PICHA: Heshima aliyopewa Victor Wanyama na kamati ya Kata ya Ubungo
Kamati ya Kata ya Ubungo ikiongozwa na Meya wa Ubungo Boniface Jacob wameamua kumpa zawadi ya heshima mchezaji wa Tottenham Hotspurs na nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama jina lake litumike katika mtaa, hiyo wakati wa mapumziko wa game ya Sports Extra Ndondo Cup 2017.
Kuanzia leo Jumamosi ya June 24 2017 mtaa wa viwandani ambao
unaelekea maeneo ya uwanja wa Kinesi Sinza utakuwa unajulikana kwa jina
la Victor Wanyama kwa heshima ya mchezaji huyo ambaye ni mfano wa kuigwa
Afrika Mashariki, Wanyama leo alikuwa ni miongoni mwa watanzania
waliyojitokeza kuangalia game ya Ndondo Cup 2017 kati ya Faru Jeuri
dhidi ya Kauzu FC.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Victor Mugubi Wanyama ni miongoni mwa
wachezaji waliyoisaidia Tottenham Hotspurs kumaliza nafasi ya pili
katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliyomalizika.
Muro Tv Ipo Play Store…Download HAPA ,Tuwe tunakutumia habari kwa haraka zaidi,kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba:0768786851, whatsapp:0768786851
No comments:
Post a Comment