Header Ads

JANGA LINGINE LAMKUMBA YUSUF MANJI

Mfanyabiashara na diwani wa kata ya Mbagala kuu Mh. Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu baada ya kushindwa kuhudhuria vikao 9 vya Madiwani na kuvuliwa Udiwani.

Ikumbukwe Yusuf Manji sasa anakabiliwa na kesi ya kujihusisha na uuzaji na utumiaji wa Madawa ya kulevya na inasemekana vipimo vya mkojo alivyofanyiwa vilithibitisha ni kweli anajihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya, na amekuwa akirudishwa mahakamani mara kwa mara kutokana na muendelezo wa kesi hiyo iliyomfanya kushindwa kuhudhuria vikao hivyo 9 vya madiwani na kuvuliwa Cheo hicho cha Udiwani. 

No comments:

Powered by Blogger.