Header Ads

Rais wa Vanuatu afariki ghafla kufuatia mshutuko wa moyo

MuroTV

Rais wa Vanuatu afariki ghafla kufuatia mshutuko wa moyo



Vanuatu President Baldwin Lonsdale speaks at a press conference at Vanuatu International Airport
Haki miliki ya picha
Image caBaldwin Lonsdale

Rais wa Vanuatu Baldwin Lonsdale amefariki kutoana na mshutuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 67.
Bwana Lonsdale, ambaye ni kasisi wa kianglikana, amekuwa kiongozi wa kisiwa hicho cha Pacific tangu Septemba mwaka 2014.
  • Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres afariki
Gazeti la Daily Post nchini Vanuatu, lilisema kuwa alifariki ghafla kwenye mji mkuu Port Vila, muda mfupi baada ya usiku wa maane siku ya Jumamosi.
Map of Vanuatu


Image captionVanuatu

Akiwa rais Bwana Lonsdale aliongoza ujenzi mpya wa maeneo ya kisiwa hicho kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Pam, kilichosababisha watu 75,000 kukosa makao mwezi Machi mwaka 2015.
Mwezi Oktoba mwaka huo huo aliapa kupambana na ufisadi nchini Vanuatu, baada ya sakata iliyomhusisha makamu wake.
  • Rais wa zamani wa FIFA afariki dunia
Makamu wake alijiondolea mashtaka pamoja na wabunge wengine 13 wakati Bwana Lonsdale alikuwa nje ya nchi, hatua ambayo aliifuta wakati alirejea nchini

Muro Tv Ipo Play Store…Download HAPA ,Tuwe tunakutumia habari kwa haraka zaidi,kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba:0768786851, whatsapp:0768786851
 Download Hpa

No comments:

Powered by Blogger.