Malinzi atuma salamu za rambi rambi msiba wa Ally Yanga
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, Jamal Emil Malinzi
ametuma salamu za rambi rambi kwa uongozi wa klabu ya Yanga SC, familia,
ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Ally Yanga ambaye amefariki dunia
Juni 20 mwaka huu.
Jamal Malinzi
amepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha shabiki
maarufu wa Young Africans, Ally Mohammed anayefahamika zaidi kwa jina la
Ally Yanga, kilichotokea jana Jumanne Juni 20, 2017 kwa ajali ya gari
iliyotokea mkoani Dodoma.Katika salamu za rambirambi kwa uongozi wa Young Africans, familia,
ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Ally Yanga ambako Rais Malinzi
amewaasa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao na kwa
huzuni amewafariji akisema: “Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake
tutarejea.”
| Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi |

No comments:
Post a Comment