Mwenyekiti Uvccm wilayani Arusha awapongeza wawekezaji kwa uzalendo wanaonyesha
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha mjini amewapongeza wawekezaji
wazalendo wanaosaidia maendeleo ya wananchi wanaowazunguka Mwenyekiti
huyo ameyasema hayo leo Kata ya Themi alipomtembelea mwenyekiti wa mtaa
wa Kambarage Ancleus Karata ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu wilaya
ya Arusha mjini
Mwenyekiti karata amemtembeza Mh: Munisi kwenye miradi mbali mbali ya
mendeleo ambayo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mradi wa maji
ambao umefadhiliwa na SUN FLAG umemaliza tatizo la maji kwa 96%
Pia vivuko ambavyo vimejengwa kwa nguvu za wananchi na kimoja kikubwa
kinachounganisha kata ya Engutoto na Themi kilichofadhiliwa na
wawekezaji SOLNIL ARUSHA SUNDRIERS pamoja na HANS PAUL
Mh Munisi akizungumza kwenye ziara hiyo alisema
" Nawaonya, Chadema waache kutembea kwenye miradi ambayo siyo ilani yao
wao walishindwa vibaya uchaguzi mkuu 2015 wenyehaki yakutembelea na
kuhoji juu ya miradi ya maendeleo ni CCM maana sisi ndiyo wananchi
waliingia mkataba na sisi 2015 -2020 na uchaguzi ujao watakuja kutuuliza
sisi CCM na siyo chadema "
" Hata hivyo ninawapongeza sana wilaya ya Ubungo kwa kuwazuia Chadema
kwenda kwenye miradi wao wasubirie siku wakijaga kushinda miaka mia
ijayo ndiyo waje kukagua siyo sasa kwasasa ni sisi ccm"

No comments:
Post a Comment