Header Ads

BREAKING: Cheick Tiote: Mchezaji wa zamani wa Newcastle afariki dunia

MuroTV

Cheick Tiote: Mchezaji wa zamani wa Newcastle afariki dunia

05 June, 2017

Cheick Tiote Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United Cheick Tiote amefariki dunia akiwa an miaka 30 baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China, msemaji wa mchezaji huyo amesema.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikaa miaka saba Newcastle na kuwachezea mechi 138 ligini.
Alihamia klabu ya Beijing Enterprises mwezi Februari.
"Ni kwa huzuni kubwa ambapo ninathibitisha kwamba Cheick Tiote alifariki mapema leo baada ya kuzimia wakati wa mazoezi," msemaji wake alisema.
"Hatuwezi kusema zaidi kwa sasa na tunaomba kwamba familia yake iheshimiwe kipindi hiki kigumu. Tunaomba maombi yenu."
Tiote alizaliwa Ivory Coast na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.Bemba Ba ni miongoni mwa wachezaji waliotuma rambirambi  Bemba Ba ni miongoni mwa wachezaji waliotuma rambirambi
Alianza uchezaji wake wa soka ya kulipwa Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht mwaka 2005 kabla ya kuhamia FC Twente ya Uholanzi ambapo alicheza mechi 86 na kushinda taji la ligi ya Eredivisie msimu wa 2009-10 chini ya meneja Steve McLaren.
Tiote, ambaye ni kiungo wa kati mkabaji, kisha alihamia Newcastle mwaka 2010 kwa £3.5m.Cheick Tiote 
Mwaka 2011, alifunga bao linalokumbukwa sana alipowasaidia Newcastle United kujikwamua kutoka 4-0 chini Ligi ya Premia dhidi ya Arsenal na kutoka sare.

MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati 

 Image may contain: text

KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; 

Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
          : prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv

 

No comments:

Powered by Blogger.