UWANJA AMBAO SERENGETI BOYS WANADHANIWA KUWEKA HISTORIA MPYA LEO
Michezo
PICHA 6: Uwanja ambao Serengeti Boys wanaweza kuweka historia Leo
Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kesho May 21 2017 itacheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B wa kuwania nafasi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya AFCON U-17 dhidi ya Niger katika uwanja wa Port Gentil uliyopo katika kisiwa cha Port Gentil.

Serengeti Boys watacheza katika uwanja huu ambao ulitumika katika michezo ya fainali za AFCON
za wakubwa walizocheza mwezi January mwaka huu, hivyo watahitaji sare
au ushindi ili wafuzu kucheza nusu fainali ya , uwanja huo ulijengwa
2015 na unauwezo wa kuchukua mashabiki 20000.

Serengeti Boys leo watacheza uwanja huu wa
Port Gentil na kama watashinda au kupata sare ya aina yoyote ile
wataweka rekodi ya kushiriki na kuingia nusu fainali ya michuano ya
AFCON kwa mara ya kwanza katika historia, hivyo watapata nafasi ya
kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la vijana moja kwa moja kufuatia
matokeo hayo, michuano ambayo itachezwa India mwishoni mwa mwaka huu.


No comments:
Post a Comment