Header Ads

UPEPO MKALI WA KUSI KUIKUMBA PWANI YA TANZANIA

MuroTv

Upepo mkali wa Kusi kuikumba pwani ya Tanzania

30 Mai 2017
Pwani ya Tanzania
UPEPO mkali wa KUSI wenye kasi ya kilometa 40 kwa saa unataraji kuvuma na kusababisha mawimbi yenye ukubwa wa mita mbili.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo huo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania. Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga kwa upande wa Tanzania Bara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba kwa upande wa Zanzibar itakumbwa zaidi na upepo huo.
"Msukumo wa upepo wa Kusi unatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania," ilisema taarifa ya TMA. Tahadhari kubnwa imetolewa kwa wavuvi na watumiaji wengine wa bahari hasa maeneo yaliyotajwa ili kuepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika.
Hali hiyo ya hewa inatarajiwa kuwepo hadi kufikia kesho 31 Mei,2017.

No comments:

Powered by Blogger.